Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM, Amos Makalla, amedai kuwa wana Karatu hawajui Dk. Wilbroad Slaa amehamia chama gani.
Makalla ameyasema hayo leo Juni 5,2025, wakati akizungumza wilayani Karatu, mkoani Arusha katika mkutano wa hadhara, akiendelea na ziara yake ya siku saba inayohusisha mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
“Wangapi walisikia Dk. Slaa amerudi CHADEMA, hakuna. CHADEMA kimesambaratika, hawana wagombea wa kutosha, hawakuwa na maandalizi na wahawa fedha ya kuingia katika uchaguzi na Rais Samia amewafilisi hoja zao zote walikuwa wakipiga kelele, Rais Samia amefanya.
“Ndio maana wakasema kichaka cha kujificha ni No Reforms No Election, lakini ndani yake wamechoka, hali yao ni mbaya, No Reforms hawana hoja eti mabadiliko yafanyike ndio uchaguzi ufanyike, hii ni hoja dhaifu. Mabadiliko yamefanyika,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED