Mwanzilishi wa CHADEMA Digital atua ACT Wazalendo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:08 PM Jun 03 2025
Mwanzilishi wa CHADEMA Digital atua ACT Wazalendo
Picha: Mpigapicha Wetu
Mwanzilishi wa CHADEMA Digital atua ACT Wazalendo

Mmoja wa waanzilishi wa CHADEMA Digital, Glory Tausi, amejiunga rasmi na Chama cha ACT Wazalendo. Glory amepokelewa leo Juni 03, 2025 katika Makao Makuu ya chama hicho na kuongozwa na Katibu Mkuu, Ado Shaibu.

Akizungumza baada ya kupokelewa, Glory amesema amevutiwa na sera makini za ACT Wazalendo pamoja na utekelezaji wa vitendo wa sera ya jinsia ndani ya chama hicho. Ametoa pongezi kwa ACT Wazalendo kwa kuwaamini wanawake na kuwapa nafasi za uongozi katika ngazi za juu.

"ACT Wazalendo si chama kinachoongea tu kuhusu usawa wa kijinsia, bali kinatekeleza kwa vitendo. Hiki ndicho chama ambacho wanawake wana nafasi ya kweli ya kushiriki katika uongozi." amesema Glory.


Ujio wa Glory ndani ya ACT Wazalendo unaonekana kuwa sehemu ya mikakati ya chama hicho kujiimarisha kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.

Glory Tausi.