Katika hafla ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Ubungo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Albert Msando, ameupokea Mwenge na kuwapongeza wavijana wanaokimbiza Mwenge huo kwa uzalendo wao pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kinondoni kwa ushirikiano wao katika shughuli hiyo muhimu ya kitaifa.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Albert Msando, alizungumza wakati wa ukaguzi wa Mradi wa Barabara ya Kibwegere – Mpiji Magohe, akieleza kuwa barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 1.4 imejengwa kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 2.8 (2,764,260,330.14).
Aidha, Mluu wa wilya ya Kinondoni, Saad Mtambule, wakati wa kuukabidhi Mwenge huo ameeleza kuwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa zaidi ya shilingi trilioni nne kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ndani ya Wilaya ya Kinondoni, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo ameeleza Miradi saba yenye zaidi ya bilioni 8.2 inayotembelewa na Mwenge ikiwa ni pamoja na ,
1. Mradi wa Barabara ya Kibwegere – Mpiji Magohe
Gharama: TZS 2,764,260,330.14
Urefu: Kilomita 1.4
Eneo: Kata ya Mpiji Magohe
2. Mradi wa Ujenzi wa Pampu ya Maji (DAWASA)
Gharama: TZS 4,256,774,774,451.00
Eneo: Kata ya Kwembe
3. Mradi wa Nishati Safi (Shule ya Dsm Girls)
Gharama: TZS 23,983,820.00
Eneo: Kata ya Kwembe
4. Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa na Matundu 8 ya Vyoo
Gharama: TZS 144,188,300.00
Shule: Mbezi Inn Secondary
Eneo: Kata ya Mbezi
5. Mradi wa Vijana (Asilimia 10)
Gharama: TZS 50,000,000.00
Eneo: Kata ya Sinza
6. Mradi wa Jengo la Upasuaji na Wodi ya Wazazi
Gharama: TZS 398,390,352.00
Kituo cha Afya: Makurumla
Eneo: Kata ya Makurumla
7. Mradi wa Uboreshaji wa Soko la Mabibo
Gharama: TZS 600,000,000.00
Eneo: Kata ya Mabibo
Miradi hii ni sehemu ya juhudi kubwa za Serikali katika kuboresha huduma za kijamii, miundombinu, na kuinua maisha ya wananchi. Kupitia Mwenge wa Uhuru, wananchi wameweza kushuhudia maendeleo ya kweli yanayogusa maisha yao ya kila siku.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED