Ujenzi wa mradi wa maji wa Ziwa Victoria kwenye umbari wa kilometa 75 kutoka Manispaa ya Kahama mpaka Halmashauri ya Ushetu mkoani Shinyanga, umefikia asilimia 17 ya utekelezaji wake huku ukitarajia kuwahudumia wakazi zaidi ya 189,000 utakapokamilika ifikapo mwakani.
Aidha, mradi huo unatekelezwa na Mkandarasi Sihotech Engineering Co.ltd ya jijini Dar es Salaamu kwa kushirikiana na Kampuni ya Mpole Construction and Co.ltd ya Iringi kwa gharama ya Sh.bilioni 44 na umbali kilometa 25 kati ya 60 za bomba zimeshalazwa ardhini.
Akieleza utekelezaji wa mradi huo leo, Msimamizi wa mradi kutoka RUWASA mbele ya Mwenyekiti wake wa bodi Taifa, Suzana Gogadi amesema, mkandarasi ameshafikisha bomba na vifungashio vyake asilimia 73 na kwa kasi aliyonayo mradi ukamilika ndani ya muda uliopangwa.
“Mradi huu umefikia asilimia 17 ya utekelezaji wake na sasa kazi zinazofanyika ni ujenzi wa matanki matatu yenye ujazo wa lita 500,000, lita 300,000 pamoja na lita 100,000 na kilometa 25 kati 60 za bomba zimeshalazwa ardhi na kazi bado inaendelea”Ameongeza Gogadi.
Amesema, utakapokamilika utasaidia kupunguza ugonjwa wa kuumwa matumbo, vipigo kwa wanawake na mimba na ndoa za utotoni mashuleni hasa kwa wanafunzi wa kike, walikuwa wakitumia muda mwingi kutafuta huduma ya maji umbali mrefu na kukutana na vishawishi njiani.
Awali Diwani wa kata ya Ulowa kunapojengwa matanki ya maji, Gabriela Kimaro wanalazimika kununua ndoo au dumu la maji la lita 20 kwa Sh.500 mpaka 1,000 gharama ambayo ni kubwa kulinganisha na vipato vyao na wakati wa masika wanachangia maji na wanyama.
Mwenyekiti wa Bodi ya RUWASA, Ruth Koya ameridhishwa na ujenzi wa mradi huo kwani mkandarasi ameweza kufikisha bomba pamoja na vifungashio vyake kwa asilimia 73 huku akiwa ameshalazama bomba kilometa 25 kati ya 75 zinazohitajika na kufikia asilimia 17 ya utekelezaji wake.
Amesema, Rais Dk. Samia Suluhu Hassani wakati anaingia madarakani kwa mara ya kwanza moja ya ajenda yake ilikuwa ni kumtua mama ndoo kichwani na hii ndio sababu kunamiradi mingi ya maji inaendelea kutekeleza nchini na kuwataka itakapokamilika kuitunza ili izidi kuwanufaisha.
Hata hivyo amempongeza mkandarasi kwa hatua aliyofikia sasa kwani baadhi yao wamekuwa wakifikisha vifaa eneo la kazi hasa bomba ila wanasahau vifungashia vyake hali ambayo inachukua muda kukamilisha miradi isipokuwa yeye amefikisha vifaa vyote kwa wakata mmoja.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED