Katika jamii yoyote inayotaka maendeleo ya kweli na ya kudumu, ushiriki wa wanawake katika siasa ni jambo la msingi. Kwa Tanzania, idadi ya wanawake ni zaidi ya nusu ya raia wote, lakini kwa muda mrefu ushiriki wao kwenye siasa umekuwa mdogo.
Ni changamoto gani zinazowakwamisha? Ni madhara gani yatatokea kutokana na kukosekana kwao katika zoezi hilo? Nini kifanyike ku- chochea ushiriki wao? Kura Yangu Nguvu Yangu ni safu ya kila wiki inaleta mijadala yenye tija, mitazamo, tafiti na simulizi halisi zinazoone- sha kuwa siasa ni uwanja wa kila raia bila kujali jinsi. Leo safu inaangalia umuhimu wa wanawake kushiriki kwenye siasa, endelea....
Kwa nini ushiriki wa wanawake kwenye siasa ni muhimu? Ni kwa sababu demokrasia ya kweli haipaswi kuwa dhana ya kisheria au mfumo wa upigaji kura tu, bali ni mfumo shirikishi unaotoa nafasi sawa kwa kila mtu kushiriki katika mchakato wa uamuzi wa kisiasa bila kujali jinsi, dini, hali ya uchumi, au ulemavu. Katika demokrasia ya kweli, kila kundi kwenye jamii lina sauti, thamani na nafasi ya kushiriki kikamilifu kwa usawa katika mchakato wa kisiasa.
Kwa Tanzania kundi kubwa la watu ni wanawake. Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, zaidi ya nusu ya raia ni wanawake. Yaani kati ya Watanzania 61,741,120, wanawake ni 31,687,990 ambayo ni asilimia 51,wakati wanaumeni 30,053,130 sawa na asilimia 49.
Licha ya hatua zinazochukuliwa na serikali pamoja na wa- dau wengine kuhimiza ushiriki wa wanawake katika siasa, mwitikio ni mdogo, hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa maendeleo ya demokrasia nchini, kutokana na ukweli kwamba hakuna demokrasia inayoweza kuwa kamili iwapo zaidi ya nusu ya wananchi katika taifa husika, hawashiriki kikamilifu katika siasa na hasa kwenye mchakato muhimu wa kuamua nani apewa mamlaka ya uongozi.
Ushiriki wa wanawake kwenye saisa huleta sauti, uzoefu na mitazamo tofauti wakati wa kujadili masuala mbalimbali yanayowagusa moja kwa moja wananchi. Wanawake, hasa wa vijijini, huathiriwa zaidi na changamoto kama kukosa maji, huduma bora za afya na kuelemewa na majukumu ya familia.
Wanawake huleta uelewa wa moja kwa moja wa mata- tizo ya wananchi. Ushiriki wao unaongeza ubora wa sera na mipango ya maendeleo kwani maoni yao yanaakisi hali halisi inayoendelea katika jamii. Kwa hali hiyo, kukosekana kwenye siasa huwaondolea uwezekano wa kuchaguliwa kuwa viongozi na hatimaye kushiriki moja kwa moja kwenye nafasi za kufanya uamuzi.
KUAKISI UHALISIA
`Sauti za wanawake kwenye siasa huakisi hali halisi inayoendelea katika jamii na zinapokosekana kwenye vyombo vya uamuzi, mitazamo yao kwenye sera, uzoefu wao juu ya changamoto zinazowakabili na pia maoni ya namna bora ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto hizo, vinakosekana pia.
Kadhalika, ushiriki katika mchakato wa kidemokrasia wa makundi yote yaliyoko katika jamii, unachochea uwajibikaji. Ushahidi unaonyesha wanawake wanaposhirikishwa katika utungaji wa sera, serikali inawajibika katika kuyaainisha na kuyatatua masuala ya kijamii.
Wanawake ni mawakala wa mabadiliko katika familia na jamii. Wanapopewa nafasi ya kushiriki katika siasa na uongozi, hucho- chea mabadiliko chanya katika usawa wa kijinsia, elimu, afya na ustawi wa familia. Kukosekana kwa wanawake katika siasa ni ku- poteza fursa ya kutumia uwezo wao katika kujenga jamii yenye usawa na mshikamano.
Viongozi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, wanatambua umuhimu wa ushiriki wa wa- nawake kwenye siasa na wameku- wa wakisisitiza hilo katika hotuba zao.
Rais wa kwanza mwanamke Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, mara kadhaa amekuwa akisisitiza umuhimu wa wanawake kwenye siasa na uongozi. Februari mwaka huu, alikaririwa akiwahimiza Watanzania kupuuza dhana potofu kwamba mwanamke ni mtu wa nyumbani pekee na hawezi kuwa kiongozi. Alisisitiza pia kuwa wanawake wana uwezo sawa na wanaume katika nafasi mbalimbali za uongozi.
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi mkuu, hivyo niwaombe wanawake mjitokeze kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali za uongozi sawa na wanaume. Pia, hakikisheni mnaandikishwa katika daftari la wapigakura ili muwe na sifa ya kuchagua na kuchaguliwa,” Rais Samia alikaririwa akisema wakati akiwapongeza wahitimu 110 wa mahafali ya 10 ya Programu ya Mwanamke Kiongozi.
“Ushiriki mkubwa wa wanawake katika siasa utawawezesha kuleta mabadiliko ya maana katika demokrasia, na kudumisha juhudi za uwezeshaji na uwakilishi wa wanawake.” Ellen Johnson Sirleaf, aliyekuwa rais wa Liberia, na rais wa kwanza mwanamke kuchaguli wa kidemokrasia barani Afrika, aliwahi kukaririwa akisema.
Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2022 alisisitiza umuhimu wa uwakilishi wa wanawake kwenye vyombo vya kutunga sheria na ushiriki wao wa moja kwa moja katika michakato ya kisiasa kama jambo la msingi kwa mabadiliko ya kidemokrasia yenye maana.
Bibi Titi Mohamed, mmoja wa mashujaa wa uhuru wa taifa hili, aliweka msingi wa ushiriki wa wa- nawake katika siasa za Tanzania. Kama mwenyekiti wa kwanza wa Jumuiya ya Wanawake ya TANU, alihamasisha kinamama kushiriki katika harakati za ukombozi, akionyesha kuwa wanawake walikuwa sehemu muhimu ya mabadiliko ya kijamii na kisiasa. Juhudi zake ziliimarisha ushirikiano wa wanawake katika maan- damano, mikutano ya kisiasa, na uchangiaji rasilimali kwa TANU.
Umoja wa Mataifa pia una- tambua umuhimu wa ushiriki wa wanawake katika siasa. UN Women inasisitiza kuwa ushiriki wa wanawake katika michakato ya kidemokrasia ni muhimu kwa maendeleo ya jamii na kwamba kuondoa vikwazo vinavyowakabili wanawake na kuwapa fursa sawa, kunaweza kujenga jamii yenye usawa na maendeleo endelevu.
Lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu linasisitiza kuwapo kwa usawa wa kijinsia, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa wanawake katika siasa.
ITAENDELEA............
Maswali ya kufikirisha
Mambo gani yanaweza kushawishi wanawake kushiriki kwenye siasa?
Tuma majibu yako kupitia mitandao yetu ya kijamii,
Instagram na facebook: @JoyceBazira
LinkedIn: DrJoyce Bazira
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED