Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) limefanya maboresho ya Liturujia katika baadhi ya vipengele ikiwemo kipengele cha matangazo ambapo awali viongozi waliruhusiwa kutoa neno na sasa haitakuwa hivyo tena.
Mabadiliko hayo yametoa katazo kwa kipengele hicho na kuanzia sasa wageni ikiwemo viongozi wa kiserikali hawatoruhusiwa kuzungumza ndani ya Kanisa Katoliki "Hakutakuwa na hotuba za kupongezana, isipokuwa tu Mwadhimishaji (Paroko, Padri kama ni tukio la kiparokia, Askofu wa jimbo kama ni tukio la jimbo, Rais wa TEC kama ni tukio la kitaifa) atatambua kwa ufupi uwepo wa wageni wa kidini, kiserikali, kijamii na waalikwa wote bila kuwapa nafasi ya kuongea, kutoa hotuba wala kusalimia"-imesema sehemu ya taarifa hiyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED