Polisi: Tumewakamata watu kadhaa kanisani kwa Gwajima

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:26 PM Jun 03 2025
Polisi: Tumewakamata watu kadhaa kanisani kwa Gwajima
Picha: Imani Nathaniel
Polisi: Tumewakamata watu kadhaa kanisani kwa Gwajima

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, Jumanne Muliro amesema Jeshi la Polisi linawashikilia watu kadhaa kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo Ubungo, kutokana na kile alichoeleza walizuia jeshi hilo kutekeleza majukumu yake.

"Wakati tukielekeza nini cha kufanya, kuna baadhi ya watu walifanya mambo ya kutoelewa, ilibidi tuwachukue na tunaendelea kuzungumza nao kujua kweli walikuwa hawaelewi au walikuwa wanakataa tu ili kusababisha fujo." amesema Kamanda Muliro na kuongeza kuwa;


“Sisi jukumu letu ni kuona tunaitekeleza Sheria, kama (Askofu Josephat Gwajima) akitaka shughuli ziendelee kufanyika basi afuate utaratibu wa Kisheria ikiwa ni pamoja na kukata rufaa kwa mamlaka za Kisheria zilizowekwa."


Kauli hiyo ya Kamanda Muliro, ameitoa mapema leo Juni 03,2025 wakati akizungumza na chombo kimoja cha habari kuhusu taarifa ya jeshi hilo kuzingira Kanisa la Ufufuo na Uzima usiku wa kuamkia leo. 

Hali ilivyokuwa katika Kanisa la Ufufuo na Uzima mapema ya leo.