Hatimaye, wanafunzi watatu wanaodaiwa kumdhalilisha mwanafunzi mwenzao wa Chuo Kikuu Ardhi, Magnificat Kimario, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Wanafunzi hao walifikishwa mahakamani leo kufuatia tukio lililojitokeza Aprili 20, 2025, ambapo video inayowaonesha wasichana wakigombana ilisambaa mitandaoni na kuzua mjadala mkubwa wa kitaifa. Katika video hiyo, jina la mtu anayefahamika kwa jina la Mwemba Burton Mwemba, maarufu kama Mwijaku, lilitajwa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi iliyotolewa Aprili 24, 2025, watuhumiwa hao walitiwa nguvuni na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Wanafunzi waliotajwa katika taarifa hiyo ni:
Aidha, Jeshi la Polisi lilithibitisha kuwa limemuhoji pia Mwemba Burton Mwemba (Mwijaku) kuhusiana na tuhuma hizo, ingawa haijafahamika moja kwa moja kama naye atafunguliwa mashtaka au la.
Kwa sasa, watuhumiwa hao wapo chini ya ulinzi wa Polisi wakisubiri taratibu za kisheria kuendelea.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED