PSSSF inavyochangia uchumi wa nchi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:05 PM May 30 2025
Elimu ya Hifadhi ya Jamii ikitolewa kwa wanafunzi wa sekondari Tanga wakati wa Maonesho ya Biashara na Utalii.
Picha: Mpigapicha Wetu
Elimu ya Hifadhi ya Jamii ikitolewa kwa wanafunzi wa sekondari Tanga wakati wa Maonesho ya Biashara na Utalii.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) unashiriki kikamilifu katika kukuza uchumi wa nchi kupitia uwekezaji wake katika sekta ya kilimo, biashara, teknolojia na utalii.

Hayo yameelezwa katika Maonesho ya 12 ya Biashara na Utalii yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Mwahako, jijini Tanga. 

Afisa Uhusiano wa PSSSF, Regina Kumba, akizungumza na wakazi wa jiji hilo waliofika katika banda la PSSSF, amesema PSSSF inashiriki Maonesho hayo kuonesha uwekezaji wa Mfuko huo katika sekta hizo lakini pia kusogeza huduma kwa wakazi wa Tanga kupitia maonesho hayo.

“Mbali na huduma ya mafao kwa wanachama wetu, Mfuko unawekeza katika kilimo na uzalishaji, PSSSF imewekeza katika Kiwanda cha Kimataifa cha Bidhaa za Ngozi Kilimanjaro (KLICL) kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro na Ranchi na Machinjio ya kisasa iliyopo Nguru Mkoani Morogoro. Uwekezaji huu unaongeza thamani ya mazao ya wakulima lakini pia kutoa huduma ya upatikanaji wa bidhaa hiyo kwa urahisi,” amefafanua.

Amesema kupitia uwekezaji wa majengo marefu na ya kisiasa ya PSSSF, imesaidia kupendezesha miji mikubwa hapa nchini kama vile Dar es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma na hivyo kuvutia watalii.

“Kubwa ni kwamba uwekezaji huu katika majengo umetoa fursa za upangishaji wa ofisi, maduka lakini pia makazi, majengo haya ni mazuri yanapendezesha miji yetu.”

Katika eneo la teknolojia, PSSSF, imepiga hatua kubwa ambapo kwa sasa huduma zote zinatolewa kwa njia ya Mtandao kupitia PSSSF Kidijitali, ambapo mwanachama anaweza kujihudumia yeye mwenyewe kupitia simu janja au kompyuta akiwa mahali popote na wakati wowote.

3