Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa 2025 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wamewasili na kushiriki kikao hicho kinachofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre, jijini Dodoma.
Mkutano huo maalum umehudhuriwa pia na wawakilishi wa vyama rafiki kutoka nchi mbalimbali za Afrika, mabalozi, viongozi wa serikali, pamoja na wawakilishi wa Watanzania waishio nje ya nchi (Diaspora).
Miongoni mwa ajenda kuu za mkutano huo ni tathmini ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020, pamoja na uzinduzi rasmi wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2025, ambayo itaongoza mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
Aidha, mkutano huo unatarajiwa kumtangaza rasmi mrithi wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, ambaye anamaliza muda wake wa uongozi ndani ya chama.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED