Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati, imeendelea kutoa hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Singida na Iringa sanjari na kuvutia uwekezaji wa bidhaa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia.
Hamasa hiyo imetolewa na Meneja wa EWURA, Kanda ya Kati, Mha. Hawa Lweno, kupitia vipindi vya redio mkoani Singida na Iringa pamoja na semina kwa mama lishe, waendesha bodaboda na wasambazaji wa gesi ya kupikia (LPG), iliyofanyika kati 27 na 29 Mei, 2025.
“ Lengo letu ni kuhakikisha watumiaji wa gesi ya kupikia wanazingatia masuala ya usalama, afya na utunzaji wa mazingira pamoja na kuhakikisha watoa huduma tunaowadhibiti wanafuata na kutii masharti ya leseni zao” amesisitiza Mha. Lweno.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED