Wanafunzi 10,300 waliopata mimba warejeshwa shuleni

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 03:14 PM May 27 2025
news
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.

Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, jumla ya wanafunzi 10,300 waliopata ujauzito wamerudishwa shule na kuendelea na masomo yao.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda, amesema hayo leo Mei 27, jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya wizara hiyo.

“Hadi sasa kwa mujibu wa takwimu ni wanafunzi 10,300 ambao ndio wamerejeshwa shule baada kupata mimba na kuendelea na masomo yao na wengine wamefanya vizuri sana, kumekuwepo na changamoto kadhaa lakini zinaendelea kushughulikiwa lengo letu ni kuona hakuna mtoto anayepata mimba akiwa shule lakini pia hatupaswi kuzuia aliyepata mimba kupata haki yake ya kusoma,”amesema