Mgombea urais kupitia Chama cha Sauti ya Umma (SAU), Majalio Kyara, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuchaguliwa kuongoza nchi serikali yake itatoa vifaa bure kwa walemavu wa aina zote ili viwasaidia katika maisha.
Akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Singida eneo la soko kuu la Singida,alivitaja vifaa vitakavyotolewa bure na serikali yake kwa walemavu kuwa viti mwendo, mashine za nukta nundu na fimbo nyeupe kwa wasioona.
“Ndugu zetu hawa walemavu hawakupenda kuzaliwa wakiwa na ulemavu hivyo ni jukumu letu kama taifa kuwasaidia ili na wao waweze kufurahia maisha yao wakiwa kama watanzania wenzetu,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED