Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, ameahidi wananchi wa Wilayani Muheza, mkoani Tanga, kuja na mpango wa kufufua viwanda vya chai na kukuza kilimo biashara.
Akizungumza leo Septemba 29, 2025, na wananchi wa Muheza, akiendelea na ziara za kampeni, Dk. Samia ameahidi, kulifanyia kazi ombi la mbunge kuongeza thamani mazao ili kupata soko.
Amesema watalifanyia kazi kwa kuja na kongani za kila wilaya, ambapo kwa Muheza wataviweka vya kuongeza thamani na usindikaji matunda na mazao ya viungo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED