Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema akiingia Ikulu, atasitisha utaratibu wa serikali wa kuchukua maeneo ya wananchi na kuyahifadhi, mpaka pale atakapojiridhisha kwamba yanatosheleza mahitaji ya wananchi.
"Maeneo yote yaliyoporwa kwa wananchi yakatengwa kama hifadhi, nitayarejesha ili yatumike kwenye kilimo na ufugaji,"amesema Mwalimu.
Amesema utaratibu wa sasa wa kuchukua maeneo ya wananchi na kuyahifadhi wakati hayatoshi mahitaji ya wananchi ni kuendelea kuongeza shida na umasikini kwa wananchi hao.
Amesema wananchi wanapokosa maeneo ya kilimo wakati yale yaliyopo yamehifadhiwa ni kuwakosea na ni kukosa utu.
"Yaani inawezekanaje unachukua ardhi ya wananchi unaihifadhi kwa ajili ya wanyama wakati wananchi wanataabika kupata maeneo ya kilimo na ufugaji, hii haikubaliki."
Amesema hayo leo kwenye mkutano wa kampeni kwenye mji wa Madibila, Mbarali mkoani Mbeya wakati akiomba ridhaa ya kuchaguliwa kuiiongoza Tanzania Oktoba 29 meal huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED