Mgombea urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu amesema, mwaka huu yuko tayari kupita mtaa kwa mtaa, kijiji kwa kijiji, kitongoji kwa kitongoji kukusanya kura mpaka kieleweke.
Amesema mwaka huu, ni 'bampa kwa bampa' 'kusaka' kura mpaka kieleweke.
Amesema katika uchaguzi mkuu mwaka huu, hayuko tayari kuacha kura hata moja bali yuko tayari kuingia hata mahali ambapo hapajawahi kuingilika kutafuta kura.
Amesema yuko tayari kuingia hata vibarazani kwenye nyumba za wananchi, kutafuta kura.
Amesema hayo akiwa eneo la Madibila, Mbarali mkoani Mbeya akiendelea na kampeni zake kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Rais wa Tanzania ifikapo Oktoba 29 mwaka huu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED