Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimeahidi kujenga na kukarabati masoko 13 katika Jimbo la Ubungo miaka mitano ijayo endapo itapewa ridhaa ya kuongoza kwa kipindi kingine.
Mgombea Mwenza wa urais wa chama hicho, Balozi Dk. John Nchimbi ametoa ahadi hiyo leo Septemba 29 katika Jimbo la Ubungo ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.
"Nimeambiwa watu wengi wa Ubungo mkitaka kufanya manunuzi yenilu mnakwenda Mlimani City na Kituo cha Biashara Ubungo. Sasa katika Ilani ya CCM miaka mitano ijayo inaeleza kutajengwa masoko ya kisasa 13 katika Wilaya ya Ububgo ili huduma mnazozifuata huko kwingineko myapata katika masoko hayo," amesema Dk. Nchimbi.
Pia amesema wataongeza uwezeshaji katika halmashauri ili kongeza kasi ya utoaji wa mikopo ya asilimia 10, sambamba na kuondoa upendelea katika utoaji wa mikopo hiyo.
Amesema kutafanyika ukarabati na uwezeshaji wa Hospitali ya Manispaa ya ubungo kwa kuongeza majengo, vifaatiba, watumishi. Ili iweze kufanya huduma za upasuaji wa dharura na kutibu magonjwa yote.
Amesema wataongeza upatikanaji wa huduma za afya kwa kujenga zahanati tatu na kituo cha afya kimoja.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED