Mkakati Dk. Samia kuwanufaisha wachimbaji

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:06 PM Sep 29 2025
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan.

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk Samia Suluhu Hassan, amedhamiria kufungua fursa za kiuchumi kwa vijana kupitia sekta ya madini, baada ya kutangaza mpango wa kuongeza eneo litakalofanyiwa utafiti kubaini uwepo wa rasilimali hiyo.

Dk Samia ameyasema hayo leo, Jumatatu Septemba 29, 2025 alipozungumza na wananchi wa Pangani mkoani Tanga, katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi.

Amesema kwa sasa eneo lililofanyiwa utafiti kubaini uwepo wa madini ni asilimia 16 pekee nchi nzima, hivyo katika miaka mitano ijayo, atahakikisha anaongeza eneo lililotafitiwa hadi kufikia asilimia 20.

“Tunataka tufanye utafiti, kujua madini gani yapo maeneo gani, ili vijana wetu, wanufaike na uchimbaji mdogomdogo waongeze kipato cha kaya zao,” amesema.