Neema wanafunzi wa vyuo vikuu na kati

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:02 PM May 12 2025
Neema wanafunzi wa vyuo vikuu na kati
Picha: Mtandao
Neema wanafunzi wa vyuo vikuu na kati

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda amesema kwa mwaka 2025/26, itaongeza idadi ya wanafunzi wanaonufaika na mikopo ya elimu ya juu kutoka 245,314 mwaka 2024/25 hadi wanafunzi 252,773.

Akiwasilisha leo bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema kwa mwaka wa kwanza watakaonufaika ni 88,320 na wanaoendelea 164,453 mwaka 2025/26.

 Pia, amesema itaendelea kutoa mikopo kwa wanafunzi  10,000 wa ngazi ya stashahada katika fani za kipaumbele ikiwamo Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati.