KWA mujibu wa utafiti daktari wa masuala ya afya ya binadamu Hamisi Kote Ali, amegundua kuwa, kugusa ardhi moja kwa moja kwa ngozi ya miguu husaidia kusawazisha chaji ya umeme mwilini.
Anasema hali hiyo inajulikana kama ‘earthing' au 'grounding’, inaweza kupunguza mfadhaiko wa akili, kuimarisha usingizi na kupunguza maumivu sugu mwilini.
Baadhi ya magonjwa unayoweza kutibu kupitia kutembea pekupeku ni kama vile, kisukari, shinikizo la damu, kuishusha hasira na kuepuka ukosefu wa kinga mwilini, anasema.
Lakini si tu faida za kimwili zinazopatikana kuna jambo la kihisia na kiroho. Kutembea peku huchochea hisia kuunganishwa na dunia.”
“Mimi hutembea miguu peku pia kama nafasi yangu ya kiroho hasa kuwa rafiki wa udongo kwani binadamu tuliumbwa kwa udongo na hapo ndipo tutakaporudi.”
“Bila shaka dunia ya leo ina changamoto zake si kila mahali ni salama kutembea miguu peku. Nilipenda kujua ameepukaje kupata majeraha tangu aanze mtindo huu wa maisha.
“Unapotembea bila viatu unamakinika zaidi kutokana na nyayo zako kugusa ardhi kinyume na ukiwa umevaa viatu, waliovaa viatu mara nyingi wanatembea barabarani na hawapo walipo kwahivyo ni vigumu kwangu kukunguwaa,” Dk. Hamisi Kote anasema.
Lakini katika enzi hizi za kisasa, teknolojia na mitindo ya maisha vinachukua nafasi kubwa katika jamii, kunao waliomwita mwendawazimu na aliyekuwa na msongo wa mawazo wanapomuona akitembea miguu peku mitaani.
“Nilipoanza kutembea bila viatu watu hasa jamii yangu ya karibu walinifikiria napitia mazito maishani, nina kasoro wengine wakinikejeli mke wangu ataniacha,” anasema Dk. Hamisi kote.
Dk. Hamisi, Mtaalamu na Mwanzilishi wa Kikundi cha Ustawi wa Garage ya Binadamu, anashauri watu kutembea bila viatu angalau nusu saa kwa siku kunaweza kuwa na athari chanya kwa afya.
Chaguo lake la maisha lisilo la kawaida limezua mijadala, huku wengi wakivu, huku wengi wakivutiwa na wazo la kuweka msingi na manufaa yake ya kiafya.
Katika dunia ya kisasa, mara nyingi tunatumia muda mwingi tukiwa tumevaa viatu, tukiwa ndani ya nyumba, maofisini au mitaani.
Chanzo: BBC
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED