Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema kupitia mradi wa kufundisha wanyama (APOPO) hususan Panyabuku wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo(SUA), panya 100 wamefundishwa na kufuzu na kupelekwa nchi mbalimbali.
Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26, Prof.Mkenda amesema panya hao wamepelekwa Angola (13), Azerbaijan (11), Cambodia (58) na Ethiopia sita (6) kwa ajili kutambua mabomu yaliyotegwa ardhini pamoja na utambuzi wa vimelea vya kifua kikuu.
Aidha, amesema panya 12 wamepelekwa nchini Marekani kama panya wa maonesho (mabalozi) kwenye shamba la wanyama.
“Utekelezaji wa mradi huo umeendelea kuijengea sifa na kuitangaza Tanzania Kimataifa ambapo panya wa Kitanzania ajulikanaye kwa jina la Ronin amevunja rekodi ya dunia kwa kutambua mabomu 109 yaliyotegwa ardhini nchini Cambodia akivunja rekodi ya panya wa Kitanzania Magawa ambaye alitambua mabomu 71 yaliyotengwa ardhini,”amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED