Kata 3,960 kutumika uchaguzi wa madiwani 2025

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 03:15 PM May 12 2025
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambengele.
Picha: Mtandao
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambengele.

Jumla ya Kata 3,960 zitatumika kwa ajili ya uchaguzi wa madiwani Tanzania bara katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambengele, amesema hayo leo Mei 12, jijini Dodoma wakati akitoa taarifa ya ugawaji wa majimbo hayo mapya ya uchaguzi na ubadilishaji wa majina.

Amesema, Kata hizo ni ongezeko la Kata mpya tano za Ngeriani na Sinoki katika halmashauri ya wilaya ya Longido na Kata ya Mupi bwawani mjini na shera katika halmashauri ya mji Rufiji ambazo zilianzishwa na Waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa.

Hata hivyo, amesema orodha ya Kata zote za Tanzania bara itachapishwa na kutangazwa kwenye gazeti la serikali.