Kaya 168,000 wanufaika na mradi lishe

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:10 PM May 12 2025
Kaya 168,000 wanufaika na mradi lishe
Picha: Mpigapicha Wetu
Kaya 168,000 wanufaika na mradi lishe

MRADI wa Kilimo na Lishe unaoitwa NOURISH Tanzania umefanikiwa kuzifikia kaya 168,000 katika wilaya 10 za mikoa ya Dodoma, Manyara, Rukwa, Singida na Songwe.

Mradi wa Kilimo na Lishe unaoitwa NOURISH Tanzania umefanikiwa kuzifikia kaya 168,000 katika wilaya 10 za mikoa ya Dodoma, Manyara, Rukwa, Singida na Songwe.

Mradi huo ni kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula na kusaidia jamii kuwa na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza tatizo la utapiamlo.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nghumbi katika Siku ya Wakulima, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeke Mayeke, amesema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na kutekelezwa na SNV kwa kushirikiana na Farm Africa, kupitia Recoda na Miico, huku ikiandaliwa Siku ya Wakulima.

Mradi huo ni kwa ajili ya kuboresha usalama wa chakula na kusaidia jamii kuwa na uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kupunguza tatizo la utapiamlo.

Akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nghumbi katika Siku ya Wakulima, Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mayeke Mayeke, amesema mradi huo unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Norway (NORAD) na kutekelezwa na SNV kwa kushirikiana na Farm Africa, kupitia Recoda na Miico, huku ikiandaliwa Siku ya Wakulima.

Amesema hadi sasa, katika mikoa hiyo mitano mradi wa NOURISH Tanzania umeimarisha kwa kiasi kikubwa mifumo ya kilimo ndani ya mwaka mmoja.

Mayeke amesema wakulima zaidi ya 6,000 wameunganishwa na wasambazaji wa pembejeo, watoa huduma 472 wa afya ya jamii wamefundishwa kuhusu lishe bora na zaidi ya wakulima viongozi 400 wamepata mafunzo ya kilimo kinachozingatia mabadiliko ya tabianchi.

Amesema mradi huo umefanikiwa kwa sehemu kubwa, wakulima wamejifunza kwa vitendo kanuni bora za kilimo chenye tija kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi kupitia mashamba darasa na kuwaunganisha wakulima wadogowadogo na makampuni yanayozalisha na kusambaza pembejeo bora za kilimo. 

"Mradi umewaongezea ujuzi wahudumu wa afya ngazi ya jamii ambao wamekua chachu katika kutoa elimu ya afya na lishe katika jamii, ili kupunguza tatizo la utapiamlo haswa udumavu kwa watoto,"
 amesema.