Miongozo mipya matumizi ya TEHAMA yaja

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:17 PM May 12 2025
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.
Picha: Mtandao
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda.

Serikali imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Elimu wa Mwaka 2024/25-2029/30 sambamba na miongozo minne kwa ajili ya utekelezaji wa mkakati huo ikiwamo na Mwongozo wa Matumizi ya Akili Unde (AI) katika Elimu 2025.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof.Adolf Mkenda ameyasema hayo bungeni leo alipokuwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2025/26.

Prof.Mkenda amesema Mwongozo wa Ujumuishi wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Shule na Vyuo vya Ualimu 2025; Mwongozo wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi 2025; Mwongozo wa Matumizi ya Teknolojia za Kidijitali katika Vyuo Vikuu 2025.

Amesema serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) 2025/26 – 2029/30 ambao utawezesha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kisekta ikiwamo utekelezaji wa sera ya elimu na mafunzo.