PSSSF yachukua alama za vidole TAPSEA kuboresha huduma

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:51 PM May 15 2025
PSSSF yachukua alama za vidole 
TAPSEA kuboresha huduma
Picha: Mpigapicha Wetu
PSSSF yachukua alama za vidole TAPSEA kuboresha huduma

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), umeshiriki katika Maonyesho ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Chama cha Waandishi Waendesha Ofisi (TAPSEA) unaofanyika katika eneo la Ngurudoto, mkoani Arusha.

PSSSF inatumia Maonesho hayo kutoa elimu ya Hifadhi ya Jamii lakini pia kutoa huduma hususan zoezi la kuchukua alama za Vidole kwa lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za Mfuko kwa wanachama wake.

Akizungumza wakati wa maonyesho, Mwakilishi wa PSSSF Baraka Kitundu alisema, "Tunaamini kuwa elimu ni msingi wa kila kitu. Tunataka kuhakikisha kuwa kila mwanachama wa TAPSEA anapata taarifa sahihi kuhusu haki zake na faida anazoweza kupata kama mwanachama wa PSSSF." 

Mkutano huu wa siku tano unawaleta pamoja wasaidizi wa waendesha ofisi kutoka sehemu mbalimbali nchini.