Huyu ndio Mwanamke Mfupi Duniani, Jyoti Amge

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 06:28 PM Apr 11 2025
Huyu ndio Mwanamke Mfupi Duniani, Jyoti Amge
Picha:Mtandao
Huyu ndio Mwanamke Mfupi Duniani, Jyoti Amge

Jyoti Kishanji Amge, alizaliwa tarehe 16 Desemba 1993, ni muigizaji kutoka India, anayejulikana kama mwanamke mfupi zaidi duniani kulingana na rekodi za Guinness World Records.

Baada ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa ya miaka 18 tarehe 16 Desemba 2011, alitangazwa rasmi kuwa mwanamke mfupi zaidi duniani akiwa na urefu wa sentimita 62.8 yaani rula mbili na sentimita 2.8 (sawa na futi 2 na inchi 3/4).

Urefu wake huu mdogo unatokana na hali ya kiafya inayoitwa primordial dwarfism, ambayo inasababisha ukuaji wa kawaida kuwa mdogo sana. Jyoti Amge si tu mwanamke mfupi, bali pia ni mfano wa uvumilivu na kujiamini, akionyesha kwamba mtu yeyote anaweza kufikia malengo yake licha ya changamoto za kiafya.

Amejulikana katika tasnia ya sinema kwa kazi zake na amekuwa ni chanzo cha inspiration kwa watu wengi duniani.Jyoti Amge amekuwa maarufu sana sio tu kwa kuwa mwanamke mfupi zaidi duniani, bali pia kwa kazi zake katika ulimwengu wa burudani. Ameonekana katika filamu nyingi, ikiwa ni pamoja na filamu za Bollywood, na pia katika kipindi maarufu cha televisheni cha Marekani, "American Horror Story: Freak Show."

Umaarufu wake umemfanya kuwa kielelezo cha uvumilivu na nguvu ya kiakili, na amekuwa akihudhuria matukio mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Kupitia mitandao ya jamii, Jyoti amekuwa akifanikisha kuwafikia mashabiki wengi, akikumbatia ujumbe wa kujithamini na kupambana na changamoto.

Aidha, umekuwa na ushawishi mkubwa katika kuhamasisha watu wenye ulemavu na kuwasaidia kujitambua, huku akionyesha kuwa kiwango cha urefu wa mtu hakiwezi kuathiri uwezo na ndoto zao. Jyoti Amge anakuza picha ya ujasiri na matumaini, na umekuwa mfano bora wa kupambana na changamoto za maisha.