Mbunge ataka maabusu maalum wanaonyonyesha, wajawazito

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 02:34 PM Apr 11 2025

Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Tofiq.
Picha: Mtandao
Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Tofiq.

Mbunge wa Viti Maalum, Fatma Tofiq, ameshauri serikali kuweka mahabusu maalum kwa ajili ya wafungwa wanao nyonyesha na wajawazito.

Toufiq ametoa ushauri bungeni leo April 11, wakati akiuliza maswali ya nyongeza kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa.

Katika maswali ya nyongeza mbunge huyo alihoji kuwa je serikali haioni sababu ya kuwa na selo maalum kwa ajili ya wanawake wanaonyonyesha na wale wajawazito.

“Swali langu la pili je wale wanawake wafungwa ambao ni wajawazito serikali inapango wowote wa lishe bora ili kusudi waweze kuimarisha afya zao,”amehoji mbunge huyo.

Akijibu maswali hayo Waziri Bashungwa, amesema wanao utaratibu maalum wa kuwahudumia akimama wajawazito wanapokuwa magerezaji.

“Kwa kupitia mapendekezo ya tume ya haki jinai kwanza tumelegeza masharti pamoja ya dhanama kwa wafungwa wanao kidhi masharti ya dhamana lakini kwa wajawazito suala la lishe ni jabo la lazima serikali inaendelea kufanya kila aina ya jitihada kuhakikisha akimama wajawazito wanapata lishe bora wanapokuwa gerezani,”amesema.