Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Damas Ndumbaro ameeleza namna alivyofurahi baada ya Dk. Emmanuel Nchimbi kutangazwa kuwa Mgombea mwenza wa Urais kwenye mkutano maalum wa CCM, Januari mwaka huu.
Akitoa salamu za Jimbo la Songea, leo Aprili 4,2025 wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) chini ya kauli mbiu ya Uchaguzi Mkuu wa Huru na haki, amesema kiongozi huyo akiwa Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini aliacha alama katika sekta mbalimbali ambazo zinagusa maisha ya wananchi.
“Siku ya Mkutano Mkuu Maalum wa CCM Dodoma nilishangilia hadi nikapanda juu ya meza baada ya jina lako kutangazwa, si kwasababu ni ndugu yangu bali nchi imepata mtu sahihi wa kumsaidia mgombe wa nafasi ya Makamu wa Rais kupitia CCM.
“Unaweza kuwa na ndugu yako lakini akawa mwehu kabisa, ila ulivyotangazwa nilijua tumepata kiongozi anayefaa sana kwa nchi yetu,”amesema Dk. Ndumbaro.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED