WANANCHI wanahitaji kuona mabadiliko ya kimaendeleo ikiwamo kwenye sekta ya afya, ili kuona matokeo ya juhudi zinazofanywa katika kufanikisha hatua za maendeleo endelevu.
Naibu Waziri wa Afya, Dk. Godwin Mollel amesema ameyasema hayo leo Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhu maadhimisho ya wiki ya afya nchini ambayo yanaendelea kufanyika katika sekta ya afya kwa matukio kwenye maeneo tofauti nchini.
Amesema uboreshaji unaofanyika kwenye sekta ya afya,utoaji wa huduma bora na vifaa vya kisasa, ikiwemo uwekezaji kwenye miundombinu na ndio mabadiliko chanya yanayohitajika.
Dk. Mollel amesema maendeleo yanayoendelea kufanywa kwenye sekta ya afya ni kielelezo mojawapo cha juhudi za Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi, ndiyo mabadiliko wanayohitaji.
Amesema mwaka huu maadhimisho haya yanafanywa nchi ikiwa imefanikiwa kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi, vifo vya mama na mtoto pamoja na idadi ya wagonjwa wanaopelekwa nje ya nchi kwa matibabu.
Dk. Mollel pia kupungua kwa vifo vinavyosababishwa na saratani kwa asilimia 78, mafanikio ambayo yamefikiwa kutokana juhudi za maboresho kadhaa ikiwamo katika mfumo wa uchunguzi wa haraka wa magonjwa hayo.
Amesema tofauti na awali vipimo vinasaidia kugundulika mapema kwa saratani, hivyo mgonjwa kuanza matibabu kwa wakati.
Awali uchunguzi wa saratani ulichukua muda mrefu kuonyesha majibu, sasa ni tofauti hatua ni kubwa kwa nchi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED