Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi za mratibu wa uchaguzi,msimamizi wa uchaguzi wilaya na msimamizi msaidizi wa jimbo.
Aidha,Mratibu wa Uchaguzi ni nafasi moja Unguja na nyingine Pemba.
Pia imeainisha sifa za kila muombaji anayetakiwa pamoja na majukumu yake.
Kwa mujibu wa tangazo lilitolewa na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa INEC,Ramadhani Kailima,kila muombaji anatakiwa kuainisha nafasi anayoomba akitaja wilaya au jimbo analotaka kufanyia kazi akiambatanisha na vyeti vya shule na maelezo ya taarifa binafsi (CV).
Taarifa hiyo iliyowekwa kwenye tovuti ya INEC imefafanua kuwa maombi hayo yatapokelewa kuanzia Aprili 3 hadi Aprili 23,2025 saa 9:30 alasiri.
"Maombi yatapokelewa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) zipelekwe Maisara kwa upande wa Unguja na Chake Chake Pemba,"amesema.
Amesema waajiriwa hao watasimamia uchaguzi wa Rais,Wabunge na Madiwani kwa Tanzania Bara kwa upande wa Tanzania Zanzibar
Kailima amesema wanaotakiwa kuomba nafasi hizo ni raia wa Tanzania, watumishi wa umma na sifa nyingine zilizoainishwa kulingana na nafasi inayoombwa.
Kailima ametaja sifa za waombaji kuwa ni watumishi wa umma wenye elimu ya shahada,stashahada ya juu au stashahada katika fani yoyote.
Aidha,awe na uzoefu wa katika masuala ya uchaguzi/uandikishaji Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Aidha,waangalizi watakuwa na majukumu manne ikiwamo kuratibu habari na taarifa mbalimbali za uchaguzi.
Wasimamizi wa uchaguzi watakuwa na majukumu sita ikiwamo kuratibu na kusimamia shughuli za uchaguzi kwenye wilaya yake.
Msimamizi msaidizi ngazi ya jimbo atakuwa na majukumu matatu ikiwamo kuwa kiungo kati ya jimbo na wilaya.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED