IMEELEZWA kuwa sekta ya Misitu inaweza kuchangia asilimia 17 ya Pato la Taifa kutoka asilimia 4 ya sasa endapo Rasilimali Misitu itatunzwa bila ya kufanyiwa uharibifu wa aina yoyote.
Hayo yamebainishwa leo, Aprili 28, 2025 mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa kikosi kazi Prof. Yonika Ngaga, katika Warsha ya mradi wa uthibitishaji wa tafiti ya mchango wa Sekta ya Misitu Tanzania kupitia uhasibu wa kijani.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 28,2025 mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa kikosi kazi Prof Yonika Ngaga, katika Warsha ya mradi wa uthibitishaji wa tafiti ya mchango wa Sekta ya Misitu Tanzania kupitia uhasibu wa kijani.
Prof. Ngaga anasema hayo ni matokeo ya tafiti zilizofanywa na kikosi kazi cha Wataalam wabobezi kilichoteuliwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania(TAFORI) na kufanyika kwenye mikoa 17 ya Tanzania Bara kutoka mwaka 2022/2023.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili Dk. Siima Bakengesa akimwakilisha Mkurugenzi wa Idara ya Misitu na Nyuki Tanzania Dk. Deusdedit Boyo anasema ukosefu wa mbinu na nyenzo bora za ufuatiliaji wa mchango kwenye sekta ya misitu katika pato la Taifa kwa kujikita katika mazao yanayoonekana kumeathiri kwa kiwango kikubwa uchangiaji wa sekta hiyo katika pato la Taifa.
Mradi huo ni mojawapo ya miradi mitano ya kimkakati ya Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) ambayo imefadhiliwa na Mifuko ya Misitu Tanzania.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED