Wakili: Nyumba ya Lissu yazingirwa na polisi, mahakama yakataa kujadili

By Grace Gurisha , Nipashe
Published at 03:22 PM Apr 28 2025
Wakili: Nyumba ya Lissu yazingirwa na polisi, mahakama yakataa kujadili
Picha: Mtandao
Wakili: Nyumba ya Lissu yazingirwa na polisi, mahakama yakataa kujadili

Wakili wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, Mpare Mpoki ameileza Mahakama kwamba nyumba ya mteja wake huyo ambae yupo mahabusu ya Ukonga imezungukwa na askari polisi.

Mpoki amedai hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Geofrey Mhini wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati kesi ya tuhuma za chuchapisha taarifa za uongo inayomkabili Lissu ilipoitwa kwa ajili ya usikilizwaji kwa hoja za upande wa Jamhuri.

"Tumepata taarifa kutoka kwa ndugu wa Lissu kwamba nyumba ya mteja wao imezungukwa na askari polisi wakati mwenyewe hayupo, yupo mahabusu," amedai Wakili Mpoki


Hata hivyo, Hakimu Mhini amesema kwamba suala hilo lipo nje ya Mahakama hawezi kulizungumzia, waendelee na usikilizwaji wa kesi.

Ilidaiwa kuwa Aprili 3,2025  jijini Dar es Salaam mshtakiwa Lissu akiwa na lengo la kulaghai umma alichapisha taarifa hizo kupitia mtandao wa YouTube ambapo maneno hayo yalisomeka ' Uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka jana , wagombea wa CHADEMA walienguliwa kwa melekezo ya Rais'.