RAIS Samia Suluhu Hassan, ameziagiza Wizara ya Fedha, Wizara ya Kilimo pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kukaa meza moja ili kuja na Sera ya Taifa ambayo itasimamia utoaji wa mikopo katika sekta ya kilimo nchini.
Rais Samia atoa maagizo kwa wizara, BoT
Rais Samia ametoa maagizo hayo leo jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Benki ya Ushirika nchini (COOP).
“Niagize sasa Wizara ya Fedha Benki kuu Wizara ya Kilimo kaeni mzungumze mfikie pahali mje na sera itakayo sijui sera ama niseme muongozo utakaotutoa kwenye hili ombwe la mikopo katika sekta ya kilimo.
“Kuwe kuna sura halisi ambayo Tanzania tunajua sera yetu inayoongozwa na benki kuu katika mikopo ya sekta ya kilimo ni hii na ni nani anafanya nini, TAD anafanya nini benki ya ushirika anafanya nini mabenki mengine yanafanya nini,”amesema
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED