"Nimepewa Taarifa na Wasaidizi wa Antipas Tundu Lissu Mughwai waliopo nyumbani kwake Tegeta, Dar es Salaam kwamba Polisi wenye silaha wamefika eneo hilo tangu alfajiri ya leo tarehe 28 Aprili 2025 na kugonga geti ili wafunguliwe, bila mafanikio.
Haijafahamika bado wana uhitaji gani wa kisheria na kimantiki, na kwa nini hawajafanya mawasiliano rasmi nasi Mawakili wa Lissu.Tutatoa Taarifa Zaidi" - Peter Kibatala, mmoja wa mawakili wa Lissu
Hata hivyo katika akaunti ya X ya Makamu Mwenyekiti CHADEMA, John Heche ameandika; "Nimezingirwa nyumbani kwangu tangu saa 10 alfajiri ya leo. Askari wakiwa na magari manne wako kwenye milango ya kuingilia."
Imeandikwa na Mwandishi Wetu- Dar es Salaam
Tembelea http://epaper.ippmedia.com kusoma gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi.
#NipasheDigital #NipasheMwangaWaJamii
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED