Watoto 78,411 kupewa chanjo ya polio wilaya ya Kahama

By Shaban Njia , Nipashe
Published at 11:24 AM Apr 26 2025
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya afya ya wilaya ya Msingi (PHC) wakati wa uzinduzi wa utoaji wa chanjo ya polio awamu ya pili leo.
PICHA: SHABAN NJIA.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya afya ya wilaya ya Msingi (PHC) wakati wa uzinduzi wa utoaji wa chanjo ya polio awamu ya pili leo.

WATOTO wenye umri wa miezi tisa na kuendelea 78,411 wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wanatarajiwa kufikiwa na kupewa chanjo ya polio kupitia vituo vya afya na huduma ya mkoba itakayowasaidia kutokupooza viungo wakati wa ukuaji wao.

Mratibu wa chanjo Halmashauri ya Ushetu, Saulo Evarist ameyabainisha haya leo wakati akitoa taarifa ya nyongeza ya chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kupooza kwa njia ya sindano (IPV2) katika kikao cha kamati ya afya ya wilaya ya Msingi (PHC) kilichofanyika Manispaa ya Kahama.

 Amesema,utoaji wa chanjo hii ni ya awamu ya pili ambayo inakwenda kuanza Mei mosi mwaka huu kwa kuwafikia watoto wa miezi tisa na kuendeela zaidi ya 78,411 kati yake Ushetu 25,071, Msalala 24,139 huku Manispaa ya Kahama wakiwa 29,201.

2.JPG 299.83 KB

 

Evarist amesema, chanjo hiyo huzuia kuenea kwa virusi vya polio, kuimarisha zaidi kinga ya mwili dhidi ya ugonjwa, kupunguza ulemavu na vifo vitokanavyo na polio na kuwataka kutohusisha ugonjwa huo na imani za kishirikana na kukimbilia kwa waganga wa jadi na kukosa kinga.

 Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dk. Yudas Ndungile amesema, awamu ya pili ya chanzo itahusisha watoto wenye umri wa miezi tisa na kuendelea na wale watakaofika kupata chanjo ya sulua watapata pia chanjo hiyo, siku ya kliniki pia wataitumia kutoa elimu juu ya umuhimu wake.

 Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mboni Mhita amewatangazia kiama watu wanaowapotosha wananchi juu ya uwepo wa chanjo ya polio na kusababisha kukimbilia kwa waganga wa jadi kuwa atawachukulia hatua za kisheria watakaopbainika kwani wanakwamisha juhudi za serikali katika kulinda afya za wananchi.

2

 

Amesema,Ofisi yake ilibaini kuwepo kwa upotoshaji wa chanjo ya polio awamu ya chanza ya baadhi ya watu wasiokuwa wadilifu kuwapotosha wananchi hasa wanaoishi pembezoni, lakini walilidhibiti na kuhakikisha watoto wote wanapata chanjo hiyo kwani ni salama na imethibitishwa kwa matumizi.

 “Madiwani tutumie mikutano yetu ya hadhara katika kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kupeleka watoto kupata chanjo hii, kwani wasipopata watapooza na kupoteza nguvu kazi ya Taifa: Serikali imekuwa ikipambana usiku na mchana kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya nzuri”Ameongeza Mhita.

 Mhita amewataka viongozi wa madhehebu ya kidini kutumia nyumba za ibada zao katika kuwaelimisha na kuwahamasisha wananchi kupeleka watoto vituo vya afya kupata chanjo hiyo na kutoa taarifa katika vyombo vya usalama kwa wale watakaobainika kupotosha umma ili wawajibishe kisheria.