Makamu Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi (CCM) Bara Stephen Wasira amewataka vijana nchini kujiandaa kuendesha chama hicho kwasababu ni chama cha kurithisha vizazi na vizazi.
Amesema miaka 60 kabla ya uhuru wa Tanganyika na kabla ya mapinduzi ya Zanzibar nchi zetu zilikuwa zinatawaliwa zote mbili na kwamba ukiwa kijana na kama hukupata nafasi ya kujua hali ilivyokuwa ukiambiwa hali haijabadilika kabisa ukikubali basi wewe sio mtafiti mzuri.
"Maana utakuwa hujui yalivyokuwa mambo kwahiyo vijana mujiandae kuendesha chama hiki maana chama chetu ni chama cha kurithisha vizazi, ndio maana tunasema kidumu chama cha mapinduzi.
"Tunasema kwa hakika kwasababu tunataka warithi wetu waandaliwe ambao ni vijana," amesema Wasira.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED