NI minne imetimu Serikali ya Awamu ya Sita ikiwa madarakani. Kuna mengi ya kisekta inaendelea kufafanuliwa kitaifa.
Ndani yake, kuna eneo moja linaloshika nguzo mbili za kifani katika biashara, Ununuzi na Ugavi (Supply Chain Management), pia Fedha.
Ili ununuzi ukamilike, unahitaji malipo yaliyo sahihi. Ili ununuzi uwe, sahihi. Nao unatajwa kuhitaji ukamilike katika kinachoitwa ‘5R’ (five rights) inayogusa: Ubora, Idadi, wakati, Bei na Chanzo au Muuzaji sahihi.
Na katika njia mbalimbali za ununuzi, mojawapo kwa kiwango kikubwa, inaitwa zabuni, ndio namna serikali hufanya ununuzi kwa sehemu kubwa.
Hiyo inatokea, huku takribani asilimia 70 ya Bajeti ya Serikali, inatajwa kutumika katika ununuzi wa umma, kwa mujibu wa mamlaka yenye dhamana serikalini na rufani zake.
Nayo ili kusimamia vilivyo, ina sheria mahususi ya ununuzi wa umma, kanuni na miongozo ya ununuzi wa umma zinazoiwezesha serikali kununua kwa namna inavyotaka.
Hapo ndipo imeunda taasisi ya wajibu huo. Mojawapo ni Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA), iliyo chini ya Wizara ya Fedha, ikaundwa kisheria tangu mwaka 2001.
Hata baada ya Sheria hiyo kufutwa, mamlaka hiyo ikahuishwa kwa Sheria ya Mwaka 2004, hali kadhalika ikahuishwa tena kupitia Sheria ya Ununuzi wa Umma Mwaka 2011, baada ya ile ya 2004 nayo kufutwa.
Mwaka 2023, Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 ikafutwa, huku PPAA ikihusishwa tena kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2023.
INAVYOFANYA KAZI
Ili kutekeleza kitaaluma ‘5R’ kwa ununuzi wa serikali, PPAA inawajibika kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi ya malalamiko au rufani zitokanazo na yao maofisa maofisa masuuli wa taasisi za umma katika michakato ya ununuzi wa umma.
Pia, PPAA inapokea na kusikiliza malalamiko ya wazabuni wasioridhika na uamuzi wa kufungiwa (blacklist) na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Kwa mujibu wa ripoti ya PPAA, katika mustakabali huo, sura ya ufanisi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inajitokeza kwa miaka minne sasa, akisisitiza usimamizi wa uwazi na uwajibikaji katika sekta ya ununuzi wa umma, kuhakikisha rasilimali za umma kwa tija, pia maendeleo ya umma kwa wakati uliokusudiwa.
Ni eneo anakorejewa Rais Dk. Samia, anakonadi misingi ya utawala bora, ikiwamo haki na usawa, miradi ya kimkakati yenye tija serikali ikiipata thamani halisi ya fedha katika ununuzi wa umma, kwa mujibu wa miongozo ya ‘5R.’
“Katika kipindi cha uongozi wa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, PPAA imeendelea kutekeleza jukumu lake kuu la utatuzi wa migogoro itokanayo na michakato ya Ununuzi wa Umma kwa haki, uwazi, uadilifu na kwa muda mfupi,” inatamka PPAA katika taarifa yake ya miaka minne ya Rais Dk. Samia.
Falsafa yake Rais ya ‘4R’ kwa maana ya; Maridhiano, Ustahimilivu, Kujenga na Usuluhushi, ununuzi wa umma umeambatanisha na falsafa yake kitaaluma 5R (idadi, ubora, muda, chanzo na muda sahihi), zimekuwa zikitumika ndani ya jukumu la PPAA, kama ifuatavyo:
USULUHUSHI (RECONCILIATION); kwa miaka minne sasa, PPAA inataja kushughulikia mashauri 171 yaliyotokana na michakato ya Ununuzi wa Umma.
Hapo ikafafanuliwa kuwa PPAA ikazuia utoaji tuzo kwa zabuni 36 kwa wazabuniwasio na uwezo wa kifedha pamoja na waliokosa sifa za kitaalamu kutekeleza zabuni husika.
PPAA inaeleza kuwa ”hatua hiyo iliepusha utekelezaji usioridhisha wa miradi unaosababisha upotevu wa fedha za umma na kuchelewesha maendeleo stahiki kwa wananchi.
Kukiendelezwa wasifu wa usuluhishi kutoka kwa Rais Dk. Samia, ikahimzia “usuluhishi wa migogoro hauwezi kupatikana penye ubaguzi na pale kuna wanaokosa fursa na haki zao za kiuchumi na kiraia. “Hivyo, kitendo… ni moja kati ya falsafa za Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.”
Eneo lingine linatajwa ni kwa PPAA kuendelea kudhibiti taasisi zinazonunua, zisikiuke taratibu za kisheria katika tathmini ya zabuni.
Kuhusu tathmini ya zabuni, katika baadhi ya mashauri, PPAA ilibaini ukiukwaji taratibu za tathimini zilizofanywa na taasisi za ununuzi ikiwemo kutozingatia vigezo vilivyowekwa katika kabrasha la zabuni au kuongezwa vigezo vipya ambavyo havikuwapo awali.
MAGEUZI/MARIDHIANO: Hapo inatajwa serikali ya Awamu ya Sita imewezesha kutungwa upya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2023, hata kuboresha udhibiti katika ununuzi.
Pia, inatajwa hatua kuchukuliwa, inabainika ukiukwaji wa taratibu katika mchakato wa ununuzi. Hiyo ni kupitia Sheria Mpya ya Ununuzi wa Umma:
Ndani yake kuna namna ya kupunguza muda wa kushughulikia malalamiko au rufani zinazotokana na michakato ya ununuzi wa umma, Mfano, muda wa kusubiri malalamiko ya wazabuni kabla ya kutoa tuzo, umepunguzwa kutoka siku saba za kazi hadi tano.
“Hautajumuisha njia za ununuzi ambazo hazihitaji ushindani (single source, minor value procurement na shopping),” inatamka PPAA katika taarifa yake.
Katika namna ya kushughulikia rufani hizo, PPAA nayo imepewa muda kisheria wa kushughulikia malalamiko au rufani, kwamba ni siku 40 hadi 45.
Eneo lingine linatajwa ni kuwekwa masharti ya lazima kwa taasisi zinazonunua kutekeleza hilo kupitia mfumo wa kieletroniki, kukitajwa kuwa
‘moduli’ rafiki na inayookoa muda.
Ikumbukwe, mageuzi kama hayo yameshafanyika katika mifumo ya fedha serikaliini.
Maboresho hayo ya kitaalum, kusaka ‘4R’ za Rais, pia 5R za kuwezesha taaluma, Mamlaka ya Rufani- PPAA, kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma, ilitoa mafunzo kwa wadau 913 wa mikoa; Dar es Salaam, Tanga, Morogoro na Pwani yaliyofanyika Dar es Salaam mwezi Mei 2024.
Pia, katika Kanda ya Ziwa Februari mwaka huu, ikagusa mikoa Mwanza, Shinyanga, Kagera, Musoma, Geita na Simiyu yaliyofanyika Jijini Mwanza.
Hayo yakawahusisha maafisa ununuzi, wakuu wa vitengo vya ununuzi, wakuu wa vitengo vya sheria, maofisa sheria, Tehama, Mawakili na wazabuni.
Pia, ndio darasa la Tehama mpya katika ununuzi ikafika jijini Mwanza kwa wazabuni na taasisi nunuzi za mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwamo Mwanza, Shinyanga, Kagera, Musoma, Geita na Simiyu.
Waziri mwenye dhamana ya fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, katika hotuba yake iliyosomwa na Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Dk. Fredrick Mwakibinga, akaeleza rasmi kwa matumizi hayo ya Tehama, kuna faida: kuokoa muda na gharama wakati wa uwasilishaji rufani na majibu ya hoja zake, huku ikipunguza mianya ya rushwa, kuongeza uwazi na uwajibikaji katika ununuzi wa umma, huku wahusika katika shauri kuweza kufuatilia na kufahamu hatua zote za uchakataji wa shauri linaloendelea.
Ni zao linalotajwa na kutungwa kwa kanuni za rufani za ununuzi wa umma, katika miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, ikitajwa kufanikishwa na vyombo kama Wizara ya Fedha, PPAA na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kukaandaliwa Kanuni za Rufani za Ununuzi wa Umma za mwaka 2024.
UJENZI MPYA (REBUILD): inatajwa kuwapo hatua ya kiserikali inayopitia PPAA kumejengwa uwezo wa wajumbe wa wadau wake wote, kuboresha mazingira ya kazi, kwa kuwapatia vifaa muhimu katika utekelezaji wa majukumu yao.
USTAHIMILIVU (RESILLIENCE): Serikali inataja kuwa, licha ya athari za kiuchumi zinazoendelea kuikumba dunia kama maradhi vile Uviko 19, vita ya Russia na Ukraine pamoja na kuadimika fedha za kigeni (dola), bado serikali inatamka imeendelea kuiwezesha PPAA kustahimili mpito huo ikitekeleza majukumu yake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED