Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho ameelekeza Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Halmashauri ya wilaya ya Songea kuhakikisha daraja la Lumecha linajengwa ndani ya kipindi kifupi na kwa ubora.
Waziri ametoa kauli hiyo jana Julai 10,2024 wakati wa ziara yake ya kutembelea Miradi ya maendeleo katika kijiji cha Liweta Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
“Serikali imetoa kiasi cha Millioni Mia nne kujenga Madaraja na akiba ya fedha itakayobaki itatumika kutengeneza barabara mpaka kijiji cha Liweta ikiwa ni pamoja na kufukia shimo lilopo katika barabara hiyo alisema,” Waziri Mhagama.
kazi ya ujenzi wa barabara ni kazi muhimu naomba wananchi msaidie katika kulinda mradi ili ujenzi ili ukamilike kwa wakati na tufungue njia zitakazochochea uchumia katika kijiji cha Liweta.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED