MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA)mkoa wa kikodi Tegeta imesema itaendelea kutoa elimu kwa walipa kodi na wafanyabiashara ili waone umuhimu wa kulipa kodi hiyo kwa hiari kukuza pato la nchi.
Kauli hiyo ilitolewa juzi na Msaidizi wa Ukaguzi na Uhiari wa Ulipaji Kodi, Maigloria Saria, baada kuwatembelea walipakodi eneo la Goba wilaya ya Kinondoni.
Alisema Mamlaka hiyo inaendelea kusogeza huduma hizo kwa Wafanyabiashara wa mkoa huo ili kuwarahisishia na kuepuka kupoteza muda mwingi kusafiri hadi Makao Makuu
Mkurugenzi wa Kampuni ya GAF International Group Limited, Flora Erasto aliipongeza serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya kufanyia biashara na kuishukuru TRA kwa kutambua kampuni yao kama walipakodi waaminifu na kuahidi kuendelea kufanya vizuri katika eneo hilo la kulipa kodi kwa serikali.
Flora alisema wataendelea kuwa waaminifu katika kutekeleza yale yote ambayo wanatakiwa kufanya katika biashara zao kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.
Mafanyakazi wa kampuni ya B&B Specialized Polyclinic, Dk. Bhavin Jani alisema wako tayari kuendelea kuinga mkono serikali kwa kulipa kodi kwa uaminifu na kwa kufuata taratibu na sheria zinazosimamia shughuli za biashara.
Dk. Jani alikipongeza kitengo cha huduma kwa wateja cha TRA kwa kuongeza ufanisi katika utatuzi wa changamoto za wateja hasa katika kipindi hiki cha mabadaliko ya teknolojia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED