Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Kamishna wa wa Polisi CP Suzan Kaganda amewasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, katika Ikulu ya nchi hiyo jijini Harare, Zimbabwe leo Juni 05,2025.
Wakati wa wasilisho hilo, Balozi Kaganda alipata wasaa wa kufanya mazungumzo na Rais Mnangagwa na kuwasilisha salaam za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan.
Masuala yaliyojadiliwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Zimbabwe hususan katika utekelezaji wa Sera ya Diplomasia ya Uchumi pamoja na ukamilishaji wa mikataba mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili kwenye sekta za afya, elimu,kilimo na madini.
Rais Mnangagwa alimhakikishia Balozi Kaganda Ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake pamoja na kuongeza kuwa, Zimbabwe inatambua na kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na Tanzania katika kuhakikisha kuwa, Taifa hilo na mataifa mengine Kusini mwa Afrika yanapata uhuru wake.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED