Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakijahudhuria hafla ya utiaji saini kanuni za maadili ya uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Katika hafla hiyo hakuna mwakilishi yeyote wa chama hicho aliyeshiriki na hivyo kukifanya chama hicho kujitoa rasmi katika mchakato wa uchaguzi.
Kanuni hizo zinasainiwa leo na vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, Serikali na Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
Vyama ambavyo vimehudhuria hafla hiyo ni ADC, Demokrasia Makini, DP, NRA, NLD, SAU,UDPD, ADA- TADEA, AAFP, CCM, CUF, ACT-Wazalendo, CHAUMMA, UMD, TLP, NCCR-Mageuzi, CCK, UDP.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED