CHADEMA Mara yakanusha ofisi zao kwenda CHAUMMA

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:25 PM Jun 05 2025
CHADEMA Mara yakanusha  ofisi zao kwenda CHAUMMA
PICHA: MTANDAO
CHADEMA Mara yakanusha ofisi zao kwenda CHAUMMA

Mwenyekiti wa HADEMA Mkoa wa Mara, Mwalimu Chacha Heche, amesema chama hicho hakina ofisi iliyotajwa kwamba ilikuwa yao bali kwasasa wanamiliki majengo yao na wapo kwenye ofisi zao, na kwamba wanaosema kwamba jengo hilo lilikuwa la CHADEMA anafanya propaganda.

Akizungumza na Nipashe Digital leo Juni 5,2025, Mwenyekiti huyo amesema wamewahi kuwa na jengo la kukodi eneo la Mukendo, Kata ya Mukendo karibu na Mara dished,lakini walihamia eneo la Saa nane ambalo kwasasa ni shule ya awali ambalo walipewa jengo na mwenyejengo wakati wanajipanga kumiliki maeneo yao.

“Wanachama wetu msikubali kuchokozeka, msiingie kwenye malumbano yoyote na chama chochote cha siasa, kwasababu tuna agenda tatu za No Reforms no election, Stronger Together na Tone Tone. Kwa hiyo hatuna sababu ya kujadili mambo ambayo jioni hayawezi kuleta majumuisho,tuna mambo ya msingi ya kujadili,”amesisitiza.

“Tulianza mchakato wa kutafuta majengo yetu tukajenga ofisi zetu maneo ya Musoma, Tarime na Bunda ambayo ingawa ujenzi haujakamilika lakini tunayatumia. CHADEMA haina jengo la kukodi.

Aidha, Heche alisema wana viwanja eneo la Rory eneo la Engri, Serengeti, Bunda Vijiji eneo la Nyamuswa na Butihama na kwamba wako kwneye jitihada za kukamilisha ujenzi, ikiwamo ni pamoja na kuwa na majengo yao katika maeneo ya Musoma Vijijini na Mwibara, huku lengo likiwa ni ifikapo 2026 kila jimbo na wilaya liwena ofisi yake.

“Majengo yote yanajengwa kwa nguvu za wananchi kupitia CHADEMA funds program. Wanachama wa Mkoa wa Mara waondoe shaka kwa kuwa hakuna jengo la CHADEMA lililochukuliwa na kwamaba hata leo (Juni 5,2025) alikuwepo ofisi na alifanya kikao cha program ya tone tone ambayo tutaizundua mkoani hapa hivi karibuni.

Mapema leo asubuhi, CHAUMMA ilileleza kuwa ofisi zilizokuwa za CHADEMA sasa ni za kwao, kisha kubadili jina na kuweka kibao kipya, jambo ambalo limepingwa vikali na CHADEMA.