Dk. Samia: Hatuna wasiwasi, tutatekeleza

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:58 PM Sep 11 2025
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan ametoa hakikisho la kuendelea kutoa ruzuku za pembejeo na mbolea kwa mazao yote ikiwemo tumbaku ambalo ndilo zao kuu mkoani Tabora.