Dk. Samia: Spika Sitta alinilea vyema uwezo na vipaji vyangu vikaonekana

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 06:55 PM Sep 11 2025
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, ameutambua mchango wa Spika wa Bunge, Hayati Samwel Sitta, katika kumlea na kumwelekeza, hatua ambayo amesema ndiyo imemsaidia kufanikisha uwezo na vipaji vyake vya sasa.

Kauli hiyo alitoa leo wakati akihutubia wananchi wa Urambo, akiendelea kunadi sera na ilani za chama chake na kuomba kura katika mikutano ya kampeni.

“Marehemu kaka yangu Sitta na Mama Sitta ni dada yangu. Marehemu kaka yangu Sitta alinilea vyema katika Bunge la Katiba. Mnajua yalitokea nini, na kule ndiko kulikoonekana uwezo wangu na vipaji vyangu. Yote chini ya mlezi wangu, kaka yangu Sitta,” amesema Dk. Samia.

Aliongeza kuwa Mama Sitta alimpokea katika Bunge la 10 akiwa mdogo, na malezi hayo yalichangia kukuza vipaji vyake kwa kipindi cha miaka mitano.

Dk. Samia aliwaeleza wananchi wa Urambo kuwa jimboni humo kwake ni nyumbani, akisisitiza uhusiano wake wa karibu na eneo hilo na wananchi wake.