Vyama vitano vya siasa vimekosa kurejesha fomu za wagombea wake wa urais katika Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) na kwa hivyo kujiuzulu katika kinyang’anyiro cha uchaguzi wa urais.
Vyama hivyo ni SAU, CCK, UMD, UDP na DP. Kwa jumla, vyama 12 kati ya 17 vilivyopata fomu vimefanikiwa kurejesha fomu zao, na zoezi hilo limefungwa leo majira ya saa 11:00 jioni.
Kati ya vyama 12 vilivyozingatia masharti, Chama cha Wananchi (CUF) kimekosa kumtambulisha mgombea wake wa urais kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya kupata wadhamini 200 kwa kila mkoa. Mgombea huyo aliishindwa kupata idadi hiyo ya wadhamini katika mkoa wa Kaskazini Unguja.
Tume ya Uchaguzi tayari imeshaweka wazi majina ya wagombea wa vyama 11 pekee, ili kutoa nafasi kwa wagombea wengine kupinga au kuwasilisha pingamizi kabla ya ZEC kutangaza rasmi majina ya wagombea kesho, Septemba 11, 2025, na kuanza kampeni za uchaguzi mkuu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED