EWURA inadhibiti mamlaka za maji 85 mijini

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:32 PM May 09 2025
 Waziri wa Maji, Jumaa Aweso
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso

Hadi kufikia Aprili, 2015, EWURA ilikuwa ikizidhibiti kiufundi na kiuchumi jumla ya mamlaka za maji na usafi wa mazingira 85 zilizoko katika miji mikuu ya mikoa, miji ya wilaya na miji midogo kupitia Sheria ya EWURA Sura Na. 414.

Sheria hiyo inaipa EWURA majukumu ya kutoa leseni kwa mamlaka za maji na kusimamia masharti ya utekelezaji wa leseni hizo; kudhibiti ubora na ufanisi wa utoaji huduma; kutathmini na kupitisha bei za huduma ya maji; na kutatua migogoro baina ya mamlaka ya maji husika na mteja.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso wakati akiwasilisha bungeni, hotuba mapendekezo ya bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka 2025/26, kuanzia Mei 8-9, 2025.