Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson, amesema kuwa mbio za marathon hazihusu ushindani pekee bali ni jukwaa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jamii.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mashindano ya riadha ya Betika Mbeya Tulia Marathon, Dk. Tulia amesema kuwa kupitia mashindano hayo, Tulia Trust — taasisi anayoiendesha — imeweza kusaidia jamii kwa kugusa sekta muhimu kama elimu na afya.
“Tulia Trust imekuwa ikitumia mapato ya mbio hizi kununua vifaa muhimu kwa shule na vituo vya afya. Hii ni njia ya kuhakikisha kuwa michezo inachangia kwa vitendo maendeleo ya jamii zetu,” alisema Dk. Tulia.
Mashindano hayo yameendelea kuwa chachu ya kuibua vipaji vya riadha huku yakiambatana na dhamira ya kusaidia makundi yenye uhitaji, na kuchochea mshikamano wa kijamii mkoani Mbeya na maeneo mengine ya Tanzania.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED