Makalla: CHADEMA yawakosesha matumaini wanachama wake

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 05:07 PM May 09 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla.
Picha: Mpigapicha Wetu
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM, CPA Amos Makalla, amesema uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) umewakosesha matumaini wanachama wake wakiwamo waliokihama na namna kinavyokwenda kitakufa mikononi mwao.

Amemweleza Makamu Mwenyekiti CHADEMA, John Heche, aliyeko katika ziara ya chama chao hivi sasa, kuwa anavyosema G50 wamehongwa, akumbuke yuko katika nyumba ya vioo hivyo asirushe mawe.

Ameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Shule ya Msingi Lupiro, Kata ya Lupiro, wilayani Ulanga katika Mkoa wa Morogoro, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku saba.

Akimjibu Heche aliyeko katika ziara ya chama chao Karagwe, Makalla  alisema, “Niliwahi kuwaambia CHADEMA wana mgogoro wakatoka wakasema hawana mgogoro. Apiongeza kuwa, “Ukipandacho utakivuna sasa hivi si siri tena kuna mgogoro mkubwa CHADEMA na Heche anatuhumu wenzake ni wanawasaliti.”

Amemwambia kuwa G55 hawajawasaliti bali uongozi wao umewakosesha matumaini na wanavyokwenda kinakwenda kufa mikononi mwao.

Amemweleza Heche kwamba asitafute mchawi kwa kuwa ni wao ndani ya chama na mipango yao wameamua CHADEMA   kwa mikono yao kife.

“Anasema eti hawa G55  wamehongwa, unalosema kuhongwa Heche kumbuka uko kwenye nyumba ya vioo,  usirushe mawe,” amesema.