Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam leo Ijumaa Julai 11, 2025 imepanga kutoa uamuzi wa maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu.
Uamuzi huo unatarajiwa kutolewa na Jaji Elizabeth Mkwizu baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili kwenye shauri hilo.
Tundu Lissu amefungua shauri la maombi akipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuahirisha usikilizwaji wa kesi ya kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni uliotolewa Juni 2, 2025.
Katika maombi hayo, Lissu anaiomba Mahakama Kuu iitishe jalada la kesi hiyo ya jinai ili ichunguze na kujiridhisha, pamoja na mambo mengine uhalali na usahihi wa mwenendo wa shauri hilo kwa tarehe hiyo.
Upande wa wajibu maombi umeweka pingamizi kuhusu maombi hayo ikiiomba mahakama iyatupilie mbali, huku ikibainisha sababu tatu. Bara la Afrika'.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED