TPF-Net Morogoro wamuinua mjane wa polisi

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 04:22 PM Jul 11 2025
TPF-Net Morogoro wamuinua mjane wa polisi
Picha:Mpigapicha Wetu
TPF-Net Morogoro wamuinua mjane wa polisi

Mtandao wa Polisi wanawake TPF-Net Mkoa wa Morogoro wametoa msaada wa vifaa vya steshenari vyenye thamani ya shilingi milioni mbili kwa mama mjane aliyekuwa ameolewa na askari wa Jeshi la Polisi.

Marehemu X- Mkaguzi Peter Kigugu alifariki akiwa anatekeleza majukumu yake Wilaya ya Kibiti Mkoa wa Pwani na kuacha mjane na mtoto mmoja.

Katibu wa TPF-Net Mkoa wa Morogoro Mkaguzi wa Polisi Zuwena Mwita amesema, vifaa hivyo vimepatikana baada ya askari kuchanga fedha kutoka kwenye mishahara yao kwa lengo la kumnyanyua mwanamke mwenzao baada ya aliyekuwa mume wake kufariki dunia.

Mjane huyo anayejulikana kwa jina la Rehema amelishukuru Jeshi la Polisi hususani TPF-Net kwa msaada huo wa vifaa vya steshenari ambavyo ataenda kufanyia biashara na kubadilisha maisha yake.

Dawati la Habari Polisi Morogoro